Breaking

Tuesday, March 17, 2020

Wabunge wa Chadema waliokuwa wamelazwa waruhusiwaDar es Salaam. Wabunge watatu wa Chadema waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Aga Khan wameruhusiwa baada ya hali zao kuendelea vizuri.

Wabunge hao Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda) na Jescar Kishoa (Viti Maalum) walilazwa tangu Ijumaa Machi 13 wakidai kupigwa na askari Magereza walipokwenda katika Gereza la Segerea kumpokea mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Akiongea na Mwananchi leo Jumanne Machi 17 Katibu wa Mdee, Martha Mtiko amesema wabunge hao waliruhusiwa Jumatatu usiku baada ya hali zao kuendelea vizuri.
"Wabunge wote wameruhusiwa jana na hali zao zinaendelea vizuri ingawa bado wana maumivu kwenye viungo,"amesema Mtiko

Katibu huyo amesema wabunge hao wanatakiwa kuripoti kituo cha polisi Stakishari kesho Jumatano ambapo walikuwa wakishikiliwa kabla ya kupewa dhamana na kupelekwa hospitali.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment