Breaking

Friday, March 27, 2020

Walioambukizwa Corona Uganda Wafikia 18


RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amesema idadi ya maambukizi nchini humo imefikia 18 baada ya vipimo 197 vilivochukuliwa jana, kuthibitisha kuwa watu wanne wameambukizwa COVID – 19.

 

Wanne hao walikuwa karantini katika hoteli zilizoainishwa na Mamlaka na wamepelekwa Hospitali ya Mulago kwa matibabu.

 

Aidha, Rais Museveni amesema wagonjwa 14 waliokuwa wamelazwa katika Miji ya Entebbe, Masaka na Mulago wanaendelea vizuri.

 

Ameongeza kuwa, mkakati wa kuwapima joto wasafiri Uwanja wa Ndege, kuwaweka karantini wanaoshukiwa kuwa na maambukizi na kuwatafuta wale ambao wamekuwa wakikimbia karantini umeonesha matokeo mazuri.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment