Breaking

Saturday, March 14, 2020

Wanawake Wengi Wanafunga na Kumuomba Wapate Mume Bora Lakini Wanashindwa Kumtambua Pale Anapokuja

Namna mojawapo ya wewe kuwa mwanamke bora na mwenye busara ni kuwa na uwezo wa kujua na kutambua mwanaume sahihi na kisha kum-keep! Wanawake wengi wanafunga na kumuomba Mungu awape mume bora lakini wanashindwa kumtambua pale anapokuja katika maisha yao.

Kwa wanaosoma Biblia, Abigaili mke wa Nabali anatabainishwa kwa namna alivyokua na uwezo kumtambua mwanaume bora. Unaambiwa Abigaili alivyosikia kwamba Daudi anakuja katika mji aliopo kulipiza kisasi kwa mumewe Nabali ambaye alimtukana Daudi, alijiandaa haraka haraka, akaandaa misosi mitamu na kukimbia kwenda kumpokea Daudi.

Na alivyoonana nae tu, alimuinamia na akazungumza maneno matamu ya kumpamba Daudi, ambayo kwayo Daudi hajawahi kuyasikia kwa mtu yeyote yule.. Alimsifia kuhusu ukuu wake (Daudi). Alimwambia kuwa ulimwengu mzima una taarifa ya namna Daudi alivyo mbabe wa vita
..alizungumza maneno matamu sana juu ya Daudi na maneno hayo yaliugandisha kabisa moyo wa Daudi. (1 Samuel 25: 18- 32). Maneno matamu yakamfanya Daudi aghairi mipango ya kumuangamiza Nabali, na akarudi alikotoka.

Wiki moja baadae, Nabali, mume wa Abigaili alivyofariki kwa kupigwa na MUNGU, Daudi akamtumia Abigail WHATSAPP MESSAGE akimwambia.."Nimesikia kuwa mumeo amefariki. Ninapita katika mji wako kesho, je utapenda upate kahawa na mimi ? Kilichotokea kinabaki kuwa historia, Abigaili akawa Malikia wa mfalme Daudi.

Kuolewa na mtu sahihi sio kuomba tu, bali inaendana na uwezo wako wa kujitambua wewe binafsi, vipaumbele vyako visivyoathiri matakwa ya huyo mwanaume, kutambua mwanaume sahihi anapokuja kwako na kufahamu ni jinsi gani utamkamata kwa maneno matamu ya kinywa chako...Yes mkamate kwa busara zitokazo kinywani mwako!

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment