Breaking

Wednesday, March 4, 2020

Watu 7 Wafariki Dunia Baada ya Lori la Dangote Kugongana na Noah


Watu saba wamefariki dunia papo hapo baada ya gari dogo aina ya Toyota Noah kugongana uso kwa uso na Lori la kampuni ya Dangote katika kijiji cha Mavuji, wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Foka Dinya, amesema hadi sasa ni miili miwili ndiyo imeweza kutambuliwa kwa majina, kutokana na vitambulisho vilivyokutwa kwenye mifuko yao.

 "Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa gari ndogo, na walikuwa ni wafanyabiashara wana mradi wao wa kutengeneza Furniture Luangwa, miili yote saba imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wawili vitambulisho vyao vilikutwa kwenye mifuko yao ya suruali ndio wameweza kufahamika, watano bado hawajafahamika" amesema Kamanda Dinya.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

Ajali hiyo ilitokea jana Machi 3, 2020, majira ya 12:00 Alfajiri, katika Kijiji cha Mavuji, Wilaya ya Kilwa, ambapo gari ndogo aina ya Hiace iligongana uso kwa uso na Lori la Kampuni ya Dangote, baada ya dereva wa gari ndogo kushindwa kuimudu vizuri gari yake wakati anakwepa shimo.

Waliotambulika ni dereva Jerome Goefrey Kileo pamoja na Christopher Kitigo.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment