Breaking

Saturday, March 28, 2020

Wawili Wapigwa RISASI Kwa Kukiuka Agizo la Kutotumia Usafiri wa Umma Uganda


Siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kusitisha huduma za usafiri wa Umma ili kuzuia maambukizi ya #CoronaVirus, watu wawili waliokuwa wakienda kazini kwa kutumia bodaboda wamepigwa risasi na Polisi

Wawili hao, Alex Olyem na Kasim Ssebude wanapatiwa matibabu Hospitali. Olyem alipigwa risasi mguuni na Ssebude alipigwa tumboni. Wametuhumiwa na Polisi kwa kukiuka maagizo ya Rais

Akizungumzia tukio hilo, Olyem amesema hakuangalia taarifa ya habari siku Rais Museveni alipotangaza hatua zinazochukuliwa kudhibiti #COVID_19 hivyo hakujua kama bodaboda zimepigwa marufuku

Ameeleza kuwa wakati wanaelekea kazini walizuiwa na Polisi walipojaribu kuuliza kosa walilofanya risasi mbili zilifyatuliwa hewani na baada ya hapo, Polisi wakaanza kuwapiga risasi

Hata hivyo, Msemaji wa Polisi Patrick Onyango, amedai wawili hao walipigwa risasi baada ya kujaribu kumshambulia Afisa wa Polisi


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment