Breaking

Friday, March 27, 2020

Wife Kanibambaa na Condom Moja, Sasa Anataka Kujua Mbili Zilikwenda Wapi

Wadau na wakuu wote hapa Jf amani iwe kwenu, nimekaa pembeni kwa muda mrefu kidogo kutokana na kuwa bize kwenye kipindi hiki cha kampeni lakini nimekuja hapa kwa dharula tu.

Nimekuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya ushindi kwenye kampeni ktk jimbo flani ambalo lipo ndanindani sana, baada ya kukaa kwa kwa zaidi ya mwezi nikiwa nje ya mji juzi wife kaja kunitembelea akiwa kaongozana na mke wa mgombea maana familia zetu marafiki, tena ujio wao ni wa kushtukiza bila taarifa (cku umepandishwa daraja wanasema alini surprise)

Mwanzo tulipoonana alikuwa ni mtu mwenye bashasha tena aliyejawa muwashawasha, nikajua hapa leo kazi ni moja kuviringishana mwanzo mwisho usiku baada ya msosi yeye akatangulia kulala sisi tukabaki na vikao vyetu vya mikakati, saa 6 hivi naingia chumbani namkuta kakaa kitandani amefura kwa hasira hadi nikapata hofu (hapo nikaona lile tumaini la kuviringishana linayeyuka taratibu)

Akaniuliza (hapo akataja jina langu halisi, hicho ndo kipimo cha kuonesha hasira zake ni kuniita kwa jina) kisha akanionesha "condom nyingine mbili zimeenda wapi" ilikuwa imebaki moja tu! moyo ukafanya paaaaah! Ujanja wote mfukoni sura ikanishuka halafu nikahisi inapauka nikahisi kama vile moyo unasinyaa pumzi zikabana moyo ukapoteza mwenendo wa mapigo yake, kwa kweli alinishtukiza kwa shambulio baya sana.

Tangu siku hiyo hadi alipondoka cku mbili baadae tulikuwa tunalala na nguo tu, hakuna maelewano jamani hebu nipeni vi mbinu viwili vi3 vya kumlainisha huyu mtu ikiwemo uongo wa level za juu maana naona anaelekea kufika kiwango cha mwisho cha uvumilivu wake, nitamkosa hivi hivi hii ni serious jamani.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment