Breaking

Sunday, March 1, 2020

Wivu wa Mapenzi...Mke Kubwa Aamua Mke Mdogo Kwa Kumchinja Shingo


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mgesi Dotto ameuawa kwa kuchinjwa shingo kwa panga, kukatwa bega na mkono kisha mwili wake kuwekwa pembeni mwa nyumba yake.

Mauaji hayo yametokea  katika kitongoji cha Nyairongo Kijiji cha Nyamantare wilayani Serengeti.

Akizungumzia mauaji hayo leo Jumapili Machi Mosi, 2020, Mkuu wa Wilaya ya Nurdin Babu amesema mauaji hayo yamefanyika Ijumaa Februari 27, 2020 Saa tatu asubuhi.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema mwili wa Mgesi umekutwa nje ya nyumba yao na mumewe aliyemtaja kwa jina la Daniel Marwa (33) maarufu Mwita.

Amesema wakati mauaji hayo yanatokea, Marwa hakuwapo nyumbani alikuwa ameenda harusini na kumuacha mkewe huyo na mke mkubwa na watoto wawili wa bi mkubwa huyo.

Mkuu huyo wa Wilaya anasema Marwa “Marwa alipofika nyumbani hapo alishtuka baada ya kukuta mkewe ameuawa na aliambiwa na majirani zake kuwa mke mkubwa ameondoka nyumbani hapo na watoto wake wawili kwa kutumia pikipiki ya kukodi.”

 “Nashindwa kulihusisha tukio hili na wivu au kitu gani, kwa sababu hawa wanawake mume wao alikuwa kwenye harusi kijiji kingine, aliporudi ndiyo akakuta mke mdogo ameuawa na mkubwa akaambiwa  ametoroka na watoto wake wawili mmoja ana miaka 10 na mdogo miaka minane, tunahisi huenda alihusika kwa nini atoroke,” amehoji Babu.

Hata hivyo, amesema habari kutoka kwa mume wake zinadai kuwa wake zake hao walikuwa na ugomvi ambao unahusishwa na wivu wa mapenzi.

Anasema mkubwa alikuwa akidai kuwa mke mdogo anapendwa zaidi kuliko yeye, “lakini anasema hakutegemea kama ingefikia hatua ya kutoana uhai.”

 "Baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Serengeti (OCD) niliwataka wafanye uchunguzi wa kina kwa kuwasiliana na wilaya nyingine ili waweze kumnasa kwa kuchunguza kwenye magari. Bahati nzuri wamefanikiwa kumkamata akiwa Bunda lakini hana watoto,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

Akizungumza na Mwananchi, mmoja wa majirani wa Marwa, anasema nao wanachunguza ili kufahamu ni dereva gani wa bodaboda aliyekodiwa na mwanamke huyo kisha watatoa taarifa polisi ili naye ahaojiwe

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment