Breaking

Monday, March 9, 2020

Young Killer na JACK Wolper Wanalipika na Kupakua Hakuna Siri Tena

Kumekuwepo na taarifa nyingi kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya rapa Young Killer na staa wa filamu Jacqueline Wolper, huenda ikawa kweli yametimia kwani wawili hao wamethibitisha hilo katika mitandao ya kijamii.


Kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, Dunia huadhimisha siku ya wanawake, ambapo Young Killer alitumia fursa hiyo kupost picha yake akiwa pamoja na Wolper katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika.

 "Yaani wewe mwanamke usiku silali, mchana Tarime, kheri ya siku ya wanawake duniani".

 Baada ya muda mfupi kupost picha hiyo naye Jacqueline Wolper akaja ku-comment kwa kuandika   "Ahsante sana Erick kwa kunipenda mimi, nakupenda pia ngosha".

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

Kwa dalili hizo na maelezo hayo, yanamaanisha wawili hao kwa sasa wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi, japokuwa wote walikuwa wanakana kipindi cha nyuma

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment