Breaking

Saturday, March 21, 2020

Zari Hassan Amrushia Jiwe Hamisa Mobeto

DAR: Ishara nyingi zinaonesha kuwa, bado mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari ‘The Boss Lady’ hajamsamehe mwanamitindo Hamisa Mobeto baada ya ‘kumrushia jiwe’ mapema wiki hii.

Ugomvi wa wawili hao ulitokana na Mobeto kukiri kuchepuka na kuzaa na baba watoto wa Zari, mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Gazeti la IJUMAA linafahamu kuwa, Zari anaamini kwamba, kama siyo Mobeto kuingilia penzi lake, angedumu na Diamond au Mondi hadi sasa.

Kwa muda mrefu sasa, Zari amekuwa akimrushia Mobeto vijembe kufuatia mrembo huyo kudaiwa bado ana ukaribu wenye maswali na Mondi.

Chanzo cha kuibuka kwa yote hayo ni baada ya mapema wiki hii, Mondi kuposti video ya Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha mama huyo wa watoto wawili akicheza Wimbo wa Jeje wa Mondi.

Jambo hilo limeibua maswali zaidi, kwani Mondi amelifanya wiki kadhaa baada ya kutengana na mzazi mwenzake mwingine, Tanasha Donna, raia wa Kenya.

Kwenye video hiyo, Mondi aliisindikiza na maneno haya; “Jeje yake mama @Deedaylan @HamisaMobetto… Global vibe. Number one song… #Jeje available on all digital platforms…link in my Bio.”

Katika hali ya sintofahamu huku ikidaiwa kuna kitu kinaendelea kati yao, haikuchukua dakika nyingi kwani Mobeto alizama kwenye ukurasa huo na kumjibu Mondi; “Baba Dee…!”

Dee ni kifupisho cha mtoto wa Mobeto aliyezaa na Mondi aitwaye Dyllan.

Hata hivyo, Zari anayeonekana kuwafuatilia kwa ukaribu, alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kicheko cha kejeli kwa wawili hao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye kipengele cha Insta Story, aliweka video akicheka na maneno yaliyosomeka;

“Hiyo siyo kelele, lakini ni kutojiamini, ni kutojithamini, unapaswa kujua tofauti.”

Kauli hiyo ya Zari haikuwahitaji mashabiki wake kuwa na digrii ya kuunganisha doti, bali walijua moja kwa moja jiwe hilo lilirushwa kwa Mobeto ambaye ndiye alikuwa ‘akitrendi’ na Mondi.


Hata hivyo, kama kawaida yao, mashabiki walimtaka Zari kupunguza hasira kwani Mondi kuwa na wanawake wengi si jambo la ajabu kwa sababu dini yake (Uislam) inamruhusu kuoa wanawake hadi wanne.

Zari alitengana na Mondi mwaka juzi baada ya kujaaliwa watoto wawili; Tiffah Dangote na Nillan kwa kile ambacho mwanamama huyo alisema ni jamaa huyo kukosa uaminifu.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment