Breaking

Wednesday, April 15, 2020

Alikiba "Mimi Sikukasirika Sikukasirika Wasanii Wangu Walivyonifuata Saa Nane Usiku na Kuniambia Wanajitoa Lebo"

Msanii wa Bongo Fleva nchini, Ali Saleh Kiba amesema ameshangazwa na kitendo cha kuondoka kwa Wasanii waliokuwa kwenye Kundi lake la Kings Music Records, Ally Killy Omary ‘Killy’ na Rasheed ‘Cheed’, amesema hakutarajia kuondoka kwa Wasanii hao katika Kundi hilo.

Kupitia Kipindi cha Tunalinda View cha Clouds TV – Kupitia Mtandao wake wa Instagram wakati akiwa ‘Live’, Kiba amesema alizungumza na Wasanii hao kwa dakika tano tu, kabla yakuomba kung’atuka kwenye Kundi hilo. “Waliniamsha usiku sana nilitaka tuongee vizuri kesho yake kwa sababu ilikuwa usiku, lakini waliniambia wanataka kutoka Kings Music, sikukasirika mimi, wana Uongozi wao (Management) pale Kings”, amefunguka Kiba.

Kiba amesema kuwa Wasanii hao hawakueleza sababu ya wao kung’atuka kwenye Kundi hilo licha yakuishi nao vizuri kwa ushirikiano wa kila aina katika masuala ya Muziki sambamba na kuwekeza kiasi kikubwa cha Pesa. Amesema Wasanii hao hawakuwa na Mkataba wowote katika Kundi hilo.

“Kiukweli hawakuwa na Mkataba wowote wakati wote walipokuwa chini Kings Music Records, hata hivyo wenyewe wamesema imetosha, wamefikia maamuzi ya kwenda kutafuta maisha yao basi hata mimi nawabariki waende wakatafute, hata Akaunti zao za YouTube watapewa na Uongozi wao (Management)”, amesema Kiba.

Kiba ameeleza kuwa Wasanii hao hawajasema wanaenda wapi, na pia amesema hajawauliza wanaelekea wapi kwa sasa baada ya uamuzi wao wakuondoka Kings Music.

ENDAPO WATAOMBA KURUDI KINGS MUSIC RECORDS INAKUAJE?

Kuhusu kuomba kurudi katika Kundi hilo, Ali Kiba amesema watajuana na Uongozi wao uliokuwa unawasimamia katika masuala yao ya muziki. “Na mimi kwangu huwa nikikataa nimekataa tu”, amesisitiza Kiba.

“Sina uhakika kwa wao kukasirishwa, mpaka kufikia hatua ya kuondoka kwenye Kundi, sina taarifa zozote za wao kuhama katika Kundi la Kings na kuhamia sehemu nyingine, sina uhakika”, ameeleza Kiba.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment