Breaking

Monday, April 27, 2020

Aunt Ezekiel Akubali Ukweli Mchungu 'Mimi na Iyobo Ndio Basi Tena'

STAA mwenye mvuto wake kwenye filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema kuwa kuachana kwake na dansa wa WCB, Moses Iyobo ni kwamba riziki imeisha, hivyo watu waache kuzungumza.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Aunt alisema suala la kuachana na mtu sio yeye peke yake ameanza na kwa wanaoamini dini, ni kwamba riziki inakuwa imeisha. Hivyo, kutafuta namna nyingine ya maisha.

“Unajua bwana kuna wakati vitu vikiisha vimeisha, hivyo mimi na Iyobo ni kwamba riziki imeisha na kamwe huwezi kuilazimisha, na sasa kila mtu anaendelea na maisha yake, kubwa zaidi ni kumuangalia mtoto wetu basi,” alisema Aunt.

STORI: Imelda Mtema

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment