Breaking

Tuesday, April 21, 2020

Baada ya Kuolewa Barnaba Ajipanga Kufuta Tatoo ya Mzazi Mwenzake

Msanii wa bongo fleva, Eliasi Barnaba maarufu Barnaba amesema mpango wake aliokuwa nao kwa sasa ni kufuta tattoo ya mama mtoto wake ambayo ameichoro mkononi mwake.

Akiiambia WasafiTv, Barnaba alisema kama mtu akiachana na mpenzi wake hana haja ya kubaki na alama yoyote kwasababu inamkubushia machungu.

Alisema alijitahidi kuvumilia lakini anaona machungu yanaongezeka hivyo anahitaji kuifuta ili kuwa sawa.

“Nimepitia maumivu na machungu mengi hivyo sihitaji kubaki na alama ya mtu ambayo nimempoteza hivyo ninampango wa kuifuta ili kumsahau kabisa".

Itakumbukwa, Barnaba na Zuu walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume na kumpa jina la #Steve. Mama Steve amefunga ndoa wikiendi iliyomalizika na mpenzi wake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment