Breaking

Saturday, April 18, 2020

Baraka "Msanii Akijichanganya na Kumtumia DM za Ajabu Mpenzi Wangu naruka naye"

Msanii Barakah The Prince ameeleza kuwa anamiliki akaunti ya mtandao wa Instagram ya mpenzi wake Najdattan, hivyo akikuta "message" yeyote ya msanii ambayo amemtumia mpenzi wake basi ataruka naye.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Barakah The Prince amesema Najdattani ameshakuwa mkewe ila bado ndoa tu, kwani hata familia yake inajua hilo kwa kuishi na mtoto wao.

"Huyu ni mke wangu ila bado ndoa tu ili kukamilisha kwa sababu familia yake inajua kwamba naishi naye kwangu, huwa nashika simu yake na namiliki akaunti yake ya mtandao wa Instagram ila sijawahi kuona ametumiwa ujumbe kutoka kwa msanii, ila siku masela wakijichanganya utaona naruka naye mmoja"  ameeleza Barakah The Prince

Pia msanii huyo amesema haoni tatizo kumiliki akaunti ya mpenzi wake kwa sababu ni jambo la kawaida na ni maamuzi aliyoamua ambayo yanaongeza uaminifu na kuaminiana.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment