Breaking

Wednesday, April 15, 2020

Bibi Aliyepigwa "Lockdown" Adai Kutaka Bia zaidi

Moja kati ya picha iliyo-trend mitandaoni ni hii ambayo inamuonesha Bibi wa miaka 94, ambaye ameshika bango ambalo linaeleza kuwa anahitaji bia zaidi, baada ya kufungiwa ndani "Lockdown" wakati wa kipindi hiKi cha ugonjwa wa Corona.Bibi huyo ambaye amejulikana kwa jina la Olive Veronesi, kutokea Mji wa Pittsburgh, Pennsylvania iliyopo Marekani, amefanikiwa kupata anachokitaka baada ya kuchangiwa makopo 150 ya bia.

Kwa mujibu wa CBS  Pittsburgh, Bibi huyo Olive Veronesi amesema anapenda sana bia kwa sababu ina virutubisho na lazima anywe kila ifikapo usiku.

"Nilikuwa nimebakiwa na makopo 12 ya bia, lazima niwe na bia kila ifikapo usiku, halafu unajua bia ina vitamini na ni nzuri kwako kama hautazidisha" amesema Bibi huyo.

Chanzo CNN.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment