Breaking

Wednesday, April 22, 2020

Bibi wa miaka 68 ajifungua Mapacha wawili, Mume wake ana miaka 70


Tumeshuhudia jinsi ambavyo tatizo la Wanawake kutopata Watoto pale wanapowahitaji linavyotuumiza au kuwaumiza Ndugu Jamaa na Marafiki na hata wengine kukata tamaa lakini Bibi huyu wa Nigeria hadithi yake nitofauti kidogo kwa sababu yeye hakukubali kukaa chini.

Unaambiwa kwa miaka 43 yeye na Mume wake walikua wakisumbuka kupata Mtoto au Watoto, hatimaye leo hii wamepata tena na habari zao kupata uzito kwenye vichwa vya habari vya kimataifa kwasababu ujio wa Watoto wao sio wa kawaida kwani Bibi huyo amejifungua akiwa na umri wa miaka 68.

Bibi huyu anaeonekana kwenye picha mwenye umri wa miaka 68 ameitwa Mama kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua Watoto wawili mapacha huko Lagos Nigeria.


Baba wa Mapacha hao Noah Adenuga mwenye umri wa miaka 70 (pichani) anasema walisumbuka sana kutafuta Mtoto mpaka kusafiri kwenda nje ya Nchi huko Uingereza ambako kunasifika kwa kuwa moja ya Nchi zilizoendelea duniani na zenye Madaktari wenye Utaalamu wa hali ya juu zaidi lakini hawakufanikiwa.

Baada ya juhudi kugonga mwamba wawili hawa waliamua kurudi nyumbani Nigeria baada ya jitihada zao kutatua tatizo la kupata ujauzito kugonga mwamba Nchini Uingereza ambako walikimbilia wakiamini kuna Wataalamu wa hali ya juu na watafanikiwa.

Mtandao wa Afrinik umeripoti kwamba Hospitali ya Chuo Kikuu cha Lagos Nigeria imesema huu ni muujiza ambapo wawili hawa walifeli majaribio ya kupata Watoto zaidi ya mara tatu kwa njia mbalimbali.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment