Breaking

Tuesday, April 7, 2020

Billnass: Sina ubavu wa kumnunulia Nandy ndinga


BAADA ya kusambaa kwa picha kwenye mitandao ya kijamii zikionesha ndinga mpya ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ na kuibuka tetesi kuwa amenunuliwa na msanii mwenzake, William Lyimo ‘Billnass’, mwenyewe amesema hana ubavu huo.  Madai hayo yaliibuka muda mfupi baada ya jamaa huyo kuweka maoni yake kwenye picha ya gari hilo aina ya BMW katika ukurasa wa Nandy kwenye Instagram; “Hiyo ni kwa ajili ya kutuletea kuku mpaka nyumbani.”

Baada ya hapo, Nandy au Nandera naye alijibu kwa mahaba mazito; “Kama unavitaka mume wangu!” Majibizano hayo ya Nandy na Billnass au Bilinenga yameibua utata upya kwenye vichwa vya mashabiki wao kwani uhusiano wao umekuwa haueleweki. Baadhi ya wananzengo walidai kuwa, Nandy atakuwa amenunuliwa gari hilo na Billnass ndiyo maana akamuita mume kwa bashasha!

Katikati ya maneno lukuki, OVER ZE WEEKEND ilimtafuta Billnass ili kujua ukweli wa mambo. Alipopatikana, Billnass alijibu kwa kucheka na kukanusha taarifa hizo kwamba hana pesa za kumnunulia Nandy gari.

“Hapana, sina ubavu huo. Sijamnunulia gari lolote Nandy. Atakuwa amenunua kwa pesa zake mwenyewe. Yale maoni niliyoandika kuwa atatuletea kuku nyumbani ni kwa sababu sasa hivi Nandy inafahamika kwamba anafanya biashara ya kuuza kuku na anatumia pikipiki, kwa hiyo mimi nilivyoona lile gari nikamtania kuwa atatuletea kwa kutumia gari na siyo pikipiki tena.

Kuhusu Nandy kumuita mume, Billnass alifunguka; “Hayo ni maneno ya kawaida, sisi tuna utani mwingi na hata mimi kuna muda mwingine namuita mke, kwa hiyo hilo lisiwashangaze sana.

“Lakini mbali na yote, mimi nampongeza sana Nandy kwa mambo anayoyafanya. Ni mwanamke ambaye anajua anachokifanya, anajielewa na anajitahidi kwa kweli na kujiheshimu pia.”

Kwa muda mrefu, Nandy na Billnass wamekuwa wakidaiwa kuwa ni wapenzi, lakini wamekuwa hawaweki mambo hadharani.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment