Breaking

Monday, April 20, 2020

BREAKING News: Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Getrude Rwakatare Afariki Dunia.Hiki hapa chanzo cha kifo cha Mama Rwakatare

Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, na mbunge kupitia tiketi ya CCM Askofu Gertrude Rwakatare amefariki Dunia Alfajiri ya leo ya Aprili 20, 2020.


Taarifa hiyo imetolewa na Mwanaye Mutta Rwakatare, wakati akizungumza na Supa Breakfast ya East Afrika Radio.

"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.

Mama Rwakatare alizaliwa Disemba 31, 1950, na hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 70.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment