Breaking

Thursday, April 2, 2020

Chidi Benz Ampa Sharti 1 Harmonize, Akishindwa basi


Mkali wa HipHop hapa nchini Chidi Benz, amesema kama atataka kufanya kazi na msanii Harmonize basi itabidi achukue jukumu la kumuandiakia na kumtafutia wazo msanii huyo.


Chid Benz amesema sasa hivi hana ukaribu na Harmonize zaidi ya kazi, na mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni katika uzinduzi wa Album yake ya Afro East siku ya Machi 13.

"Nipo karibu sana na Harmonize kama msanii ila sipo kama watu wanavyoongelea, sijawahi kufanya naye kazi na sio mbaya kama nitafanya naye ila lazima nimuandikie kwanza, akae akijua akitaka kufanya wimbo na mimi lazima nimuandikie, nimpe wazo na nimtafutie mdundo, kama akiona mbaya basi ataandika ya kwake " ameeleza Chidi Benz.

Aidha ameendelea kusema  "Naogopa kusema kama nipo karibu naye kwa sababu hata mara ya mwisho nilionana naye kwenye uzinduzi wa Album yake ya Afro East".


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment