Breaking

Saturday, April 18, 2020

Corona Tanzania: 127 Wapata Nafuu, Walioambukizwa 147 – Video

WAKATI idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona imefi kia 147 nchini kote, habari njema ni kwamba 127 kati yao wanaendelea vizuri kwani wanatembea vizuri, wanazungumza na baadhi wameanza kufanya mazoezi.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipokuwa anazungumzia mwenendo wa maambukizi ya ugonjwa huo hadi kufikia jana Aprili 17, 2020.


Waziri Ummy alisema wakati idadi sasa imefikia 147, wagonjwa 11 wamepona na kuruhusiwa huku wengine 127 wakiendelea vyema na wanne wakiwa katika hali mbaya. Alisema vipimo vya juzi (Aprili 16) katika Maabara ya Afya ya Jamii vimebaini kuwapo kwa wagonjwa wengine wapya 53

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment