Breaking

Monday, April 27, 2020

Daimond anunua hoteli ya nyota tatu, aitoa kwa seikali kutumika kama hospitali ya wagonjwa wa corona

Msanii wa muziki wa bongo Daimond platnums amenunua hotel ya kisasa yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Mikocheni na katika kipindi hiki cha janga la corona ameitoa mchango wake kwa serikaali kama itahitajika itumike kama karantini na kama itafaa kutumika kama hospitali ataitoa bure kwa serikali.

Daimond ameyasema hayo leo april 27 wakati akihojiwa kwenye redio yake ya Wasafi FM na kusema hoteli hiyo inavyumba zaidi ya 30 ambayo itasaidia kusogeza huduma karibu kuliko mloganzila ambapo pana umbali.

"Kipindi hiki cha janga la corona tutaitoa kama karantini bure na kama serikali itaona inafaa kuwa hospitali itumike kipindi hiki ili iwe raisi zaidi kuliko watu kwenda kule Mloganzila" alisema Diamond

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment