Breaking

Saturday, April 25, 2020

Fahyvanny "Sasa Hivi Napiga PICHA Kwa Bilioni Moja"


Mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva Ray Vanny , mrembo Fahima ambaye ni Mwanamitindo, amezidi kuweka wazi kuwa muonekano wake ni kitu ambacho kimekuwa kikichukua fedha zake nyingi.

Mashabiki wamekuwa wanahoji ni wapi bibie anatoa fedha za kupendeza kila wakati mtandaoni, huku haonekani katika dili kubwa za kumuingizia fedha za kufanya hayo yote.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma mrembo huyo alikaririwa akidai kuwa humgharimu zaidi ya Tsh. Milioni 3 kwa ajili ya kupiga picha ambazo ni kama matangazo kwenye kazi yake ya mitindo.

Sasa hii leo shabiki yake mmoja kwenye mtandao wa Instagram amemuuliza iwapo bado anatumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kupiga picha, naye akajibu hilo; “Niliishia kulekule, sasa hivi nipo huku kwa 1 Bilioni toka huko kwa 3 Milioni, njoo huku kwa 1 Bilioni,” Fahyvanny alimjibu shabiki huyo.

Ikumbuke Fahyvanny ambaye ni mshindi wa tuzo ya Best Dressed Lady kutoka Starqt Awards kutokea nchini Afrika Kusini, hivi karibuni aliuza baadhi ya nguo zake ambazo tayari amekwisha kuzivaa kipindi cha nyuma. Bei ya nguo hizo ilikuwa ni kunzia Tsh. 50,000 hadi 200,000 na mashabiki wake waliweza kuzinunua na kumalizika ndani ya muda mfupi.

Nini maoni yako

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment