Breaking

Monday, April 13, 2020

Godbless Lema Ashangaa Safari Za Ndege Kufutwa


Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya chama ha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameshangazwa na kitendo cha mamlaka ya usalama wa anga nchini kutangaza kuvunja safari zote za ndege za kimataifa nchini

Lema ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akidai kuwa kitendo hicho ni cha kushangaa kwani Dunia kote ndege zilisha zuiliwa kutoka isipokuwa nchini tu“Eti Tanzania yafuta safari za nje!!nje gani hiyo?takribani Dunia nzima viwanja vya ndege vimefungwa,nyie mlikuwa mnaenda wapi?au MWANZA,KIA,CHATO,JNIA ndio huku mnaita nje?Dunia ina shangaa tunavyo treat hii PANDEMIC.Hata hivyo imendikwa (Baada ya kiburi ni anguko)” ameandika Lema

Taarifa  ya kufutwa kwa safari za ndege za kimataifa kuingia nchini inakuja siku chache nara baada ya Rais Magufuli kusema  Tanzania haitofunga mipaka kutokana na ugonjwa wa Covid19

Eti Tanzania yafuta safari za nje!!nje gani hiyo?takribani Dunia nzima viwanja vya ndege vimefungwa,nyie mlikuwa mnaenda wapi?au MWANZA,KIA,CHATO,JNIA ndio huku mnaita nje?Dunia ina shangaa tunavyo treat hii PANDEMIC.Hata hivyo imendikwa "Baada ya kiburi ni anguko".
169 people are talking about this


No comments:

Post a Comment