Breaking

Wednesday, April 8, 2020

Hatimaye Ronaldinho Aachiwa Huru Gerezani

NGULI wa Soka wa Klabu ya Barcelona na Timu ya taifa ya Brazil, Ronaldinho Gaucho na kaka yake Assis Moreira wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32.

Ronaldinho na Kaka yake wamepata dhamana kwa dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7) baada ya awali kukataliwa dhamana nyepesi kwa hofu wangeweza kutoroka.

Pamoja na kupata dhamana hiyo lakini jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hotel katika mji wa Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum.

Ronaldinho ambaye aliwahi pia kuzichezea Paris Saint-Germain (PASG) na AC Milan pamoja na kaka yake walikamatwa na Polisi nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia nchini humo na Passport feki za Paraguay ambazo zinawaonesha wao kama raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment