Breaking

Monday, April 20, 2020

Hospitali ya Muhimbili Yakanusha Madai Kuwa Muuguzi Wake Amefariki Kwa Corona

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekanusha taarifa zinazosambaa kuwa Muuguzi Evodia Kapinga amefariki kwa #COVID19 na kwamba alikuwa anahudumia Wagonjwa wa #CoronaVirus

Taarifa ya Hospitali hiyo imesema, Muuguzi huyo hajawahi kuhudumia wagonjwa wa #COVID19 ila alikuwa anatoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto Muhimbili

Pia, taarifa imesema marehemu alikuwa na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua siku nyingi japo kwa maadili ya kazi hawakutaja maradhi hayo

Evodia Kapinga alizidiwa Aprili 18 akiwa nyumbani kwake Kimara na amefariki leo alfajiri, Aprili 19 akiwa hospitali ya Sinza Palestina. Taarifa imesisitiza kuwa uvumi wa kuwa amefariki kwa #CoronaVirus upuuzwe.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment