Breaking

Wednesday, April 29, 2020

Huwezi Amini Diamond Platnumz Bado Anamzimikia Sana Zari..."Thamani yako Kwangu Haitakaa Ipotee Katika Macho Yangu"

Baada ya Zari kumuita msanii Diamond deadbeat father, msanii huyo hakukimya bali ampa bonge la jibu, hii ni baada ya zari kupost ujumbe na kusema Diamond hajui wala hana shughuli la kujua wanawe wanavyoendelea.


Diamond akiwa katika mahojiano na runinga ya Wasfi alimwambia Zari kuwa thamani yake katika macho ya Diamond hitawahi badilika wala kugeuka.

“Wakatii ambapo humo katika mahusiano na muwe na watoto kuna uchungu ambao unabaki endapo mtawachana na mpenzi wako

Uchungu huo huwa unawachwa na wanawake kwa maana wao ndio wamebaki na watoto na kuwalea,niliona ujumbe huo na awali tulikuwa tunazungumza kupitia mawakili wetu

Nilimtumia ujumbe na kumwambia kuwa yeye ni mzazi kama mimi na heshima yake kwangu ndiyo ya maana.”Alisema Diamond.

Diamond alisema licha na changamoto ambazo wanapitia ana mthamini mama wa watoto wake.

”Hii ninkwa sababu alinizalia watoto wangu wa kwanza, na hata tukikosana mara ngapi thamani yake kwa macho yangu haitawahi badilika wala kushuka chini

Nilimwambia hamna haja ya kupost jumbe zingine kwenye mitandao ya kijamii kwa maana inaleta picha mbaya tulizungumza na kila mmoja wetu akatoa shida zake kwenye meza

Na tukagundua kuwa kulikuwa na shida ya mazungumzo kati ya mawakili wetu.” Aliongea.

Yote tisa kumi akimalizia alikuwa na haya ya
”Namshukuru Mola na natumai baada ya janga la corona kusaidiana kulea watoto wetu kutabadilika.” Diamond Alizungumza.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment