Breaking

Saturday, April 25, 2020

Jack WOLPER, Meja Kunta kitu na Boksi?


DAR: Licha ya kuwepo kwa janga la maambukizi ya Virusi vya Corona, mambo hayaishi mjini kwani ndiyo kwanza yanazidi kupamba moto.

Habari ya mjini kwa sasa ni kuwepo kwa tetesi kuwa mastaa wawili Bongo, Jacqueline Wolper ‘Wolperstylish’ kutoka Bongo Muvi na mkali wa Singeli, Khalid Sadick ‘Meja Kunta’ kuwa wanatoka kimapenzi.

Chanzo cha karibu na wawili hao kimeliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, vuguvugu la wawili hao lilianza baada ya kuwa na ukaribu wa aina yake na kuonekana wakiwa pamoja maeneo mbalimbali ya viunga vya Jiji la Dar.

Kama hiyo haitoshi, tetesi hizo zilitiwa chumvi na kitendo cha Wolper kuwa anaposti na kusapoti ngoma za Meja Kuta kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.

Mbali na kuziposti nyimbo hizo, pia amekuwa akijirekodi akiziimba nyimbo hizo anapokuwa dukani kwake na kuzitupia mitandaoni.

Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Meja Kunta ili kueleza kinagaubaga ukweli wa mambo kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikanusha madai hayo na kusema Wolper ni mshikaji wake tu na si vinginevyo.

“Hakuna kitu kama hicho, sina uhusiano wowote wa kimapenzi na Wolper isipokuwa sisi ni washikaji tu na kuhusu yeye kusikiliza na kuposti ngoma zangu, ni kusapoti kazi zangu kwa sababu ya ushikaji.

“Pia watu wajue mimi nina mpenzi wangu japokuwa sijawahi kumweka wazi hivyo watu hawamjui,’’ alisema Meja Kunta huku simu ya Wolper ikiita bila kupokelewa.

Stori: HAPPY MASUNGA, Ijumaa

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment