Breaking

Thursday, April 23, 2020

JPM "Kupulizia Dawa Kwenye Mabasi Huo ni Upuuzi”

“Wapo wanaotoa mawazo ya kuifunga DSM, haiwezekani kamwe, DSM ni center ambako asilimia kubwa ya mapato inapatikana, hatuwezi tu kuifunga DSM kisa corona, DSM ina Watu Million 6 hatuwezi kuwafungia, kesho tena Mwanza tuifunge hapana, hatuwezi kufanya lock down DSM”-

DSM, na Mwanza niliona mabasi yanapulizwa dawa na hasa DSM, hakuna upuliziaji dawa unaoweza kuua corona, ingekuwa pakipulizwa corona wanakufa, Nchi zinazoendelea wangemwagia Nchi zao kwa Ndege na wasingekuwa wanakufa, kule kupuliza dawa ni upuuzi tu” – JPM

“Hauwezi kuua corona kwa kupuliza dawa kwenye mabasi na mitaani ile unaua mende na wadudu wengine, ila hatujiulizi kwamba labda kupuliza ndio tunaongeza corona, maana DSM imepulizwa dawa tu na kasi ya wagonjwa imeongezeka, vyombo vya ulinzi mkachunguze nani alitoa hizo dawa”- JPM

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment