Breaking

Saturday, April 18, 2020

Killy na Cheed Wafunguka Sababu za Kumkimbia ALI Kiba na Kings Music

Wasanii Killy na Cheed ambao wamejitoa katika lebo ya Kings Music Records ambayo ipo chini ya msanii Alikiba wamesema sababu ya kujitoa kwenye menejimenti hiyo ni ushauri waliopewa kutoka kwa wazazi wao.


Wakitoa sababu hiyo kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV, wasanii hao wamesema mpango wa kujitoa waliuanza kuufikiria tangu miezi miwili iliyopita kisha wakachukua maamuzi.

"Sababu ya sisi kuondoka Kings Music ni kazi tu halafu maisha ni safari na hatua, suala la kuondoka Kings Music tumeshirikiana sisi na wazazi wetu na imechukua muda kama wa miezi miwili hadi kuchukua maamuzi , hatuwezi kurudi tena tunamuomba Mungu atusaidie tunapokwenda" amesema Killy 

Aidha kwa upande wa Cheed amesema  "Picha ambayo naiona ni kwamba menejimenti inatakiwa kutambua msanii awe vipi, kuanzia masuala ya 'brand' , malazi na makazi, kiukweli kuna mambo mengi ambayo yapo na yanayoendelea japo mengine hatuwezi kuyasema"


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment