Breaking

Thursday, April 23, 2020

Kocha Ataka Wachezaji Wamuige Mbwana Samatta

KOCHA msaidizi wa klabu ya soka ya Mtibwa Sugar, Patrick Mwangata amewaasa wachezaji nchini kumuiga nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika suala la nidhamu na uvumilivu pale wanapopata nafasi ya kwenda kujaribu maisha ya soka nje ya nchi.


Akizun-gumza na Championi Jumatano,Mwangata alisema kuwa wachezaji wengi wa Ki-bongo hawa-na uvumilivu na nidhamu ya soka na ndiyo maana wengi wao hufanya majaribio nje ya nchi na kushindwa.


“Wachezaji wengi wa Kitanzania siyo wavumilivu huku pia suala la nidhamu kwa baadhi yao likiwa ni changamoto kubwa na hii ndiyo sababu wengi wanapata nafasi ya kwenda nje kufanya majaribio lakini hurudi na visingizio vingi kama vile masuala ya masilahi au hali ya hewa kitu ambacho si sahihi.

“Kama hilo lingekuwa tatizo basi Samatta asingefi ka alipo, lakini yeye alitanguliza nidhamu na uvumilivu mwisho ametutoa kimasomaso, hivyo ni muhimu nyota wetu wakajifunza kutoka kwake na kutambua kuwa ili kufi ka mbali unahitaji nidhamu ya kutosha na uvumilivu.


“Taifa letu linahitaji nyota wengi zaidi ambao wataenda kucheza katika klabu kubwa barani Ulaya na kwingineko duniani ili kuwa na timu ya Taifa imara ambayo inaweza kupambana,” alisema Mwangata.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment