Breaking

Tuesday, April 21, 2020

Lema Amuambia Waziri wa Afya Apige Marufuku Safari za Mazishi


Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema amemshauri Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupiga marufuku safari za mazishi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

“@umwaliku safari za mazishi kutoka sehemu moja kwenda nyingine ziratibiwe au zipigwe marufuku kwani zaweza kuwa chanzo cha maambukizi Covid 19 vijijini,”.

Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akisema kuwa Tanzania mazishi ni heshima na watu wanasafiri kutoka sehemu mbalimbali za nchi hasa jamii zenye utamaduni wa kuzika kwao.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment