Breaking

Thursday, April 9, 2020

Lema "Natoka Dodoma Bungeni kwenda Arusha Kusalimia Familia Je Nitakaa Karantini Kwanza?"

Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema watu wanatoka nje ya nchi wanakaa karantini kwa sababu wanaamini nchi wanazotoka zina maambukizi ya Corona.

“Sasa ugonjwa upo ndani natoka Dodoma Bungeni kwenda Arusha kusalimia familia je nitakaa karantini kwanza,” alihoji Lema.

Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa inahitajika kufikiri sana hilo tatizo ni kubwa.

“Watu wanao toka nje ya nchi wanakaa karantini kwa sababu tuna amini kuwa nchi wanazotoka zina maambukizi ya Corona virus. Sasa ugonjwa huko ndani. Natoka bungeni kwenda Arusha kusalimia familia je nitakaa karantini kwanza. Tunapaswa kufikiri sana hili tatizo ni kubwa sana,” aliandika Lema.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment