Breaking

Saturday, April 25, 2020

Magufuli: asamehe wafungwa 3,973 , atoa ujumbe kuhusu Corona

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amewataka Watanzania kutumia siku ya kesho Aprili 26, kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na janga la virusi vya Corona.

Katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano, Mhe. Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3973, ambapo kati yao, wafungwa 3717 wamesamehewa vifungo vyao na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa mpaka kufa wamebadilishiwa adhabu.

Mhe. Rais Magufuli amesema ana matumaini kuwa wafungwa hao wamejifunza na kujirekebisha ili waungane na jamii katika kulitumikia Taifa wakiwa raia wema wanaozingatia sheria.

Aidha Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko na safari zisizo za lazima.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment