Breaking

Tuesday, April 7, 2020

Mbinu pekee atakazotumia Konde boy kumkabili Diamond na Kumuacha Kwenye Mataa


Na, Robert Heriel

Mwaka 2015 niliwahi kuandika makala inayozungumzia mbinu anayoitumia Diamond Platanum kumzima Ali Kiba, Mbinu ile niilipa jina la "UTAWIWISHAJI" Katika makala ile nilielezea kwa kina ni namna gani fomula hiyo inavyofanya kazi na namna inavyomuathiri hasimu.

Utawiwishaji ni nadharia na kanuni niliyoibuni ambayo hutumika katika mapambano ya namna yoyote ile, iwe mapambano katika vita, biashara, ndoa, dini, siasa n.k

Utawiwishaji ni kitendo cha kujiongeza, kujizalisha, kujitanua, Yaani mtu mmoja kujiongeza na kujipachua awe zaidi ya wawili. Kwa mfano mimi Taikon nijipachue tuwe zaidi ya wawili. Yaani Taikon 1, Taikon 2, Taikon 3, Taikon 4.........N.k
Hiyo unaweza iita Matrix.

Katika kumkabili adui yeyote ni lazima utumie mbinu hii ambayo haijawahi kushindwa, mbinu ambayo inatumika na watu washindi wote, iwe kwa wao kujua au kutokujua.

Mwaka 2015 nilimtahadharisha Msanii Ali Kiba kwa kumwambia kuwa endapo hata chukua hatua ya kukabiliana na Diamond katika vita vyao vya Muziki basi kuna hatari ya yeye kupotea na kupigwa vibaya na Diamond.

Ali Kiba alipuuzia, hakuona umuhimu wa yeye kutumia mbinu na fomula niliyomgea. Alikuja kuitumia mwishoni kabisa akiwa tayari amechelewa. Kwa sasa Ali Kiba hana jipya, hana uwezo wa kukabiliana na Diamond tena, hana nguvu ya kuwaambia washabiki wake na wanajeshi wake waingia vitani kwenye uwanja wa muziki. Wamepigwa vibaya mno.

Katika makala ile niliweza kutoa mifano michache kwa nchi zinazotumia fomula hiyo ingawaje nchi hizo zinaweza zisijue kama zinatumia fomula hiyo au huenda zinatumia jina jingine. Nilitoa mifano pia kwa vyama vya siasa kama CCM jinsi zinavyotumia fomula hiyo na ndio maana chama cha mapinduzi kinafanikiwa katika harakati zake.

Katika Fomula ya Utawiwishaji kuna kanuni ndogo ndogo; Nazo ni:
1. Pachua mbili kwa awamu ya kwanza
2. Pachua zaidi ya mbili katika awamu ya pili.
3. Nyausha/ Ua mbili, na zaidi katika awamu zote.

Niliandika kuwa katika nadharia ya utawiwishaji tunasema hao wote unaowapachua kutoka kwako mwenyewe ni Bandia. Hiyo nimeiita "kutengeneza adui bandia" ambao mahasimu wako watapigana nao badala ya kupigana na wewe mwenyewe yaan.

Mfano 1:
Mimi Taikon 1 nina ugomvi na mtu aitwaye Jebali.
Mimi Taikon 1 nitajipachua nitakuwa Taikon 2, Taikon 3 nk. Wakati Jebali atakuwa mwenyewe.
Neno taikon tuipe herufi T
Neno Jebali tuipe herufi J

T1 ............................... Mimi halisi
T2 ............................... Bandia anayenikaribia nguvu.
T3 .................................. Bandia anayemkaribia T2 nguvu.

T2 Huyu nitampa nafasi ya kukabiliana na J, Muda huo mimi nitakuwa nampush ili azidi kumchosha J.
;ZINGATIA, Nitakuwa namtumia T2 bila ya yeye kujua, yaani zile nguvu nilizokuwa natumia kupambana na J nitazipunguza kwani tayari yupo wa kupambana na J.

T3 kazi yake kubwa ni kumuandaa kwa ajili ya kumkabili T2 kama atanigeuka na kuondoka katika kampani yangu. T2 nitakuwa karibu naye zaidi kuliko T3 lakini nitakuwa namfanyia namfurahisha kwa kumshtukiza ili asahau na aondoe zile hisia kuwa nampendelea T2.

Kupitia mfano 1, Diamond alikuwa T1, Hamornize T2, Rayvany T3, na wengineo ambao sijawaweka kwenye Listi.
Jebali ndiye Ali Kiba.

Ali Kiba alikuja kuitumia mbinu ya Utawiwishaji wakati tayari ameshazidiwa na mshindi keshatangazwa.

Kwa sasa Ali Kiba hamuwezi hata huyo Harmonize, achilia mbali Diamond.

Kosa kubwa alilolifanya Diamond ni kujisahau katika kanuni ndogo ya Utawiwishaji inayosema:
" Tawi likishachipua juu ya shina kuu, halipaswi kugusa udongo iwe udongo wa chini, au pembeni kwani kwa kugusa udongo tawi hili linaweza kujitengenezea mizizi itakayolifanya lijitegemee" Hiyo ipo kwenye kitabu changu cha Nadharia za Taikon, sura ya pili, yenye kichwa kisemacho FOMULA YA UTAWIWISHAJI.

Diamond alimuacha Harmonize akagusana na udongo,hatimaye akaota mizizi ambayo imemfanya asimtegemee sana Diamond kwani naye anauwezo wa kujisimamia na kusaka chakula.

Zifuatazo ni mbinu anazoweza kuzitumia Harmonize kumdondosha Diamond, kwani nina uhakika kabisa Diamond hawezi kufurahia kustawi kwa Harmonize kwa kuzingatia Fomula ya utawiwishaji.

1. Atoe bidhaa ile ile aitoayo Diamond, aongeze ubunifu wake.
Konde Boy lazima atoe product ile ile anayoitoa Mond kisha aiongezee thamani. Hii tumeiona kwenye nyimbo zake nyingi, Harmonize ameweza kuiga uimbaji wa Diamond kwa kiasi kikubwa tena akaongeza ziada. Ni wazi harmonize anauwezo wa kumcopy Diamond lakini Diamond hawezi kumcopy. Kwa tunaojua muziki, Harmonize anajua kuimba kuliko Diamond, hili hata Mond mwenyewe analijua. Alichomzidi ni mikakati.

2. UMIZIZISHAJI.
Harmonize lazima atumie kanuni ya umizizishaji ili kumuondoa katika gemu Diamond. Katika kanuni hii, mtu anapaswa kuzalisha mizizi mingi chini zaidi ili kumfanya awe stable. Kupitia mizizi ni wazi Harmonize atajiongezea washabiki wengi zaidi kuliko Diamond.

Umizizishaji kwa habari za muziki, ni pale msanii anatumia zaidi soko la ndani kujitanua kwenda nje. Harmonize lazima atumie gap na kosa la kiufundi la Diamond ambalo ni kudharau soko la ndani kwa kulitoza pesa nyingi kwenye shoo za matamasha. Hii Konde boy anapaswa aitumie vizuri sana, ingawaje anapaswa asijirahisishe moja kwa moja.

Diamond kosa kuu analolifanya ni kuwa jinsi anavyokata mizizi yaani soko la ndani, ndivyo anavyofanya matawi na majani yasinyae kwa juu ya mti wake, ambao kimataifa wanayaona. Diamond asichoelewa ni kuwa mizizi yake haipo nje ya nchi bali ndani hata kama matawi yake yapo nje. Hii itampa fursa Konde boy kutumia kanuni ya umizizishaji na kummaliza Diamond kama hatokuwa mwangalifu.

3. Kuteka matawi mengine ya Diamond.
Harmonize anapaswa kuyateka matawi mengine aliyoyaacha WCB iwe kwa kuyaangusha,kuyashawishi yaungane naye, kuyashawishi yajitegemee kama yeye anavyojitegemea, kutunga propaganda na kuwafitinisha.

Hakuna asiyejua kuwa kwa sasa Diamond anatumia nguvu zaidi kwenye matawi, Diamond hana wazo jipya tena, hana muziki mpya tena, anachokifanya ni kuwatumia madogo yaani matawi yake, ndio kina mbosso na Rayvany.

Diamond kwa sasa anawahitaji zaidi watu hao kwani yeye kwa sasa hana jipya. Hawezi toa muziki wenye kuteka hisia za wengi kama ilivyo zamani.

Sishangai kuona nyimbo yoyote nzuri iwe ya Rayvany au mboso ni lazima ashirikishwe kwenye uimbaji na video. Hiyo tumeiona kwenye nyimbo zote kali za alizoimba Harmonize utamuona Diamond yumo, nyimbo zote kali alizoimba Rayvany utamuona Diamond yumo.

Lakini nyimbo yake kali usishange asipowashirikisha watoto hao. Hiyo ndivyo kanuni ya utawiwishaji inavyofanya kazi.

Hivyo Konde Boy unakazi ya kuhakikisha unayayumbisha matawi, kuyateka na kuyazima matawi ya Diamond kwa hayo ndiyo kwa sasa yanampa nguvu.

Ni tofauti na Ali Kiba ambaye angetakiwa kudeal na Diamond mwenyewe kuliko matawi yake.
Ukishakata matawi mti unabaki kama kisiki tuu kisicho tamanika kutokana na kutokuwepo kwa matawi na majani.

4. Acha Skendo Chafu
Moja ya mbinu mujarabu inayokubeba na itakayokubeba Harmonize ni ishu ya Skendo chafu. Usitoke toke hovyo na wanawake kama alivyokuwa anafanya Diamond. Hii itakufanya uheshimike sio kwa umaarufu au pesa bali utaheshimika kama mtu unayejitambua na mwenye maadili. Diamond hakuna anayemuheshimu zaidi ya kumshobokea kisa ni maarufu na pesa. Ila ni mtu asiyejitambua kwa habari za maadili.

Hata kama unamambo yako machafu jitahidi yasijulikane ili kulinda heshima yako.


Baada ya kusema hayo, nimalize kwa kusema; Muziki ni sanaa na sehemu ya ajira kwa vijana wengi. Watu washirikiane ili kufanya soko la muziki kukua. Lakini kama mtu atahitaji kutumia mbinu chafu basi ajibiwe kwa mbinu chafu.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment