Breaking

Monday, April 20, 2020

Mchekeshaji Pierre Liquid akutwa na virusi vya corona

Mchekeshaji Peter Mollel maarufu kama Pierre Liquid amebainika kuwa na maambukizi ya #COVID19 na sasa yupo Hospitali ya Amana akiendelea na matibabu

Amesema, "Nina bosi wangu wa karibu ambaye kapata ugonjwa huu na kwa kuwa mara nyingi tuko naye alinishauri na mimi nikapime kwa nia njema ili kama ninao nipate matibabu mapema na kuepuka kuwaambukiza wengine”

Ameongeza, "Nilienda hospitali ya Temeke, wakanipima ndipo nilipokutwa ninao na kuletwa hapa Amana ambapo kwa sasa ni moja ya kituo cha wagonjwa.”

Hata hivyo, amesema kuwa yeye anahisi atakuwa ameambukiziwa baa maana ndio maeneo yake ya kujidai na hivyo amewapongeza baadhi ya viongozi waliotoa tamko la kufungwa kwa baa akisema ni hatua nzuri

Amesisitiza kuwa maeneo ya baa watu kuwa makini kujikinga na ugonjwa huu ni ngumu na pia huusisha mikusanyiko ambapo mtu akiwa hajalewa anaweza kukaa mbali na watu lakini pombe zikishamuingia akili hiyo haitakuwepo tena

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment