Breaking

Friday, April 10, 2020

Meneja wa Hamisa Mobetto Nae Ajitosa Kulalamika Wimbo wa Ali Kiba Kufanyiwa Figisu Youtube

Meneja wa Hamisa Mobetto na meneja wa Alikiba wajitosa kutuhumu watu flani kwa kulalamikia views wa wimbo wa Dodo kufanyiwa figisufigisu huko YouTube -

"Naomba niongee kitu kidogo tu. Sio katika harakati za kufagilia au kutofagilia kazi za msanii au wasanii fulani. Video ya Dodo muda flani ilikuwa na viewers 1,000,000 then sasa hivi imeshuka hadi 700,000 kweli guys this is right? Mbona wabongo tunapenda sana kufanya vitu vya kipuuzi kwenye kila kitu? So viewers wanapunguzwa ili iweje? Ili wimbo uitwe mbaya au tuseme haukufikisha viewers 1m kwa siku moja?" Ameandika meneja wa Mobetto na kuongeza -

"Wasanii wa muziki na filamu wanapaswa kutafakari namna Bora ya kushindana. Kama mwenzako ana viewers 1m in 24 hours achia na wewe video ya kumzidi yeye upate 1.5m in 24 hours. So sad kwamba tunaingiza uswahili, uchawi, ujanja ujanja hadi kwenye kazi za Sanaa ambazo huamuliwa kwa macho ya watazamaji. I feel sorry for my country about these silly stupid feuds ambazo hazimsaidii mtu yeyote. BONGO TUTAFIKA KWELI?" Ameandika Max Rioba meneja wa Hamisa Mobetto
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment