Breaking

Wednesday, April 22, 2020

Msanii JayDee Asema Corona sio Ugonjwa wa Kuficha ni Vizuri Wakaweka Wazi


Msanii wa Muziki wa Bongo Flave, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady JayDee amesema Corona si kitu cha aibu mtu akipata ifichwe.

“Sio ugonjwa wa zinaa useme aliyeupata alizini kwa hiyo iwe siri kumsitiri. Hii ni ya wote,” aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter.

Msanii huyo amesema kuweka wazi kunaweza kusaidia watu kuwa makini zaidi “Mtazamo tu si lazima niwe sahihi. #staysafe,”.

” Corona si kitu cha aibu mtu akipata ifichwe, sio ugonjwa wa zinaa useme aliyeupata alizini kwa hiyo iwe siri kumsitiri. Hii ni ya wote, kuweka wazi kunaweza hata kusaidia watu kuchukulia serious na kujilinda zaidi. Mtazamo tu si lazima niwe sahihi. #staysafe,”.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment