Breaking

Sunday, April 19, 2020

Mtangazaji wa Clouds FM, Kenedy The Remedy Anusurika KIFO Kwenye Ajali Mbaya ya GARI

Kenedy the Remedy Ameandika Haya:

Mungu ni mwema mno, na siwezi kumshukuru vya kutosha kwa upendo wake na rehema juu yangu, familia yangu na wanaonizunguka, licha ya udhaifu wangu wote kanipa nafasi nyingine ya kuishi 🙏
Nawashukuru Sana wasamaria wema na Polisi walionipa msaada baada ya kupata ajali, wakanitunzia kila kitu mpaka familia yangu ilipofika.
Shukrani kwa madaktari wote kunitibu na walionifanyia upasuaji Dr. Sam, Dr. Sadot kutoka Rabinisia Memorial Hospital Tegeta na wauguzi wote walionisaidia. Shukrani za kipekee ziende kwa walionitoa uoga nikubali upasuaji Mama la mama Sylvia a.k.a mshika pesa zangu 😀, My brother Yahya a.k.a Nguli, Dr. Issac Maro toka TMH, Dr. Sizya toka Muhimbili Hospital.
Ndugu, Jamaa na Wafanyakazi wenzangu walioniombea kwa namna yoyote ile nirejee kwenye hali yangu ya kawaida pia nawashukuru 🙏
Naendelea poa ngoja nivute pumzi kidogo ntarejea kuliamsha ka kawa kwenye Familia Kubwa Kuliko XXL


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment