Breaking

Friday, April 24, 2020

Mtoto wa Mondi Amtesa Tanasha

IONGEZWE sauti au mmeshasikia kwamba Tanasha Donna anajuta kumzalia mtoto Nasibu Abdul ‘Diamond’ au Mondi?

Mwanamke huyo raia wa Kenya, hivi karibuni alikiambia chombo kimoja cha habari nchini humo miezi kadhaa baada ya uhusiano kati yake na Mondi kufa, kwamba anajutia kuzaa na msanii huyo maarufu Bongo.

 

“Nilikuwa mwangalifu nisimpende (Mondi) kupitiliza kwa sababu nilitaka kwanza kumjua zaidi tabia zake.

“Ghafla nilishtuka kuona nimekuwa mjamzito, kusema kweli sikuwa tayari kuwa mama.

“Kilichoniponza ni kwamba, sikuzingatia mzunguko wangu wa hedhi, nikajikuta nimenasa,” alisema Tanasha.

 

Mwanamke huyo alikwenda mbali zaidi na kufichua siri nzito kwamba, alipopata ujauzito alijikuta akiingiwa na mawazo ya shetani yaliyomshawishi autoe.

“Niliamini ili kuondoa tatizo ni kutoa ujauzito, lakini nashukuru Mungu

sikuyapa nafasi mawazo hayo,” alisema Tanasha alipokuwa akizungumza na chombo hicho cha habari mwishoni mwa wiki iliyopita.Aliongeza kuwa, baada ya majuto kuwa mjukuu, alijikuta hana chaguo zaidi ya kuendelea kukubaliana na matokeo.

Alisema: “Baada ya hapo, sikuwa na cha kufanya, tayari nilikuwa na mtoto na hapo sikupaswa kujiangalia mimi tu, ilitakiwa kila uamuzi lazima nimfikirie na mwanangu.

 

“Pamoja na kujitokeza kwa migogoro mingi katika uhusiano wetu, sikutaka kuchukua uamuzi wa haraka kujinasua na karaha za mapenzi, nilivumilia kwa sababu sikutaka kumlea mtoto wangu bila kuwepo baba yake.”

 

Kutokana na uzoefu wa kuwa mama wa watoto wawili aliozaa na Mondi, mwanamke mwingine Zarinnah Hassan ‘Zari’ raia wa Uganda, alijitokeza hivi karibuni na kumshauri Tanasha kuwa hapaswi kuwa kwenye majuto kwa vile kila kitu kinawezekana.

“Tanasha, wewe unazo pesa za kutosha katika mfuko wako za kumtunza mtoto wako, achana naye (Mondi) kwani yeye ni nani,” Zari aliwahi kumtumia ujumbe huu Tanasha.

 

Itakumbukwa kuwa, kabla ya Mondi kuzaa na Tanasha, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Zari na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili kabla ya kila mtu kuendelea na maisha yake.

Aidha, baada ya kumtema Zari, Mondi alijimuvuzisha kwa mrembo mwingine Mbongo; Hamisa Mobeto ambako nako alibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume na baada ya hapo, uhusiano wao uliyumbayumba.

 

Hata hivyo, kabla ya Tanasha kujutia kuzaa na Mondi, Zari alishaanika majuto yake mapema huku Hamisa naye akionesha hisia zake hasi kwa mzazi mwenzake kwa kumfikisha mahakamani kudai matunzo ya mtoto, kesi ambayo ilimalizwa kiaina miaka kadhaa iliyopita.

 

Licha ya kuwa msanii nyota kinara Bongo. Mondi hajafikia uamuzi wa kuwa na mwenza halali, jambo ambalo limekuwa likiwakera baadhi ya viongozi wake wa dini.

Katika hatua nyingine, baadhi ya watu wamemshauri Mondi kuwa makini na malezi ya watoto ili kuondoa mtazamo hasi juu yake kipindi ambacho watoto hao watakapokuwa wakubwa.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment