Breaking

Saturday, April 25, 2020

Mwanamuziki Marioo Aweka Wazi Kuhusu Kusaini Konde Gang

Msanii wa Bongofleva Marioo, amesema ni ngumu kwake kwasasa kusema atasaini Konde Gang au hawezi kusaini ila tayari ameshafanya kazi na Harmonize.


Akiongea kwenye Friday Night Live ya East Africa Television jana usiku, Marioo ameweka wazi kuwa amefanya bonge la ngoma na Harmonize hivyo mashabiki wao wakae tayari tu.

''Muda wowote tunatambulisha hilo dude na siku hiyo hakuna kusema kuwa tunatambulisha ngoma bali tunatambulisha muziki, ila kuhusu kusaini sitasema siwezi au nitasaini, lakini sikuwa na mpango wa kusainiwa na Lebal yoyote maana nina mipango yangu mikubwa'' - Marioo.

Ukiacha mchongo huo, Marioo pia amepata shavu la kufanya ngoma na Legend wa muziki wa mduara Bob Haisa, ambaye pia alikuwepo kwenye FNL. Bob Haisa ameeleza anavyomkubali Marioo hivyo hata ngoma watakayofanya itakuwa ni mali ya Marioo yeye hataki chochote.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment