Breaking

Thursday, April 2, 2020

Mwanaume Kama Unajua Huna Hela Usifanye Haya


Maisha siku zote yana pande mbili pande ya kupata na pande ya kukosa na watu wote unaowaona mtaani jua kabisa wanapitia pande zote hizi mbili za maisha hata mabilionea wakubwa dunia wamewahi kupitia hali ya kukosa, ndio kukosa hela hivyo siku zote kama wewe ni mtoto wa kiume na upo kwenye upande wa kukosa yaani unatafuta kwa sasa yaani huna hela upo zako tu mtaani na huna dili hakikisha ufanyi mambo haya ili kujilindia heshima na hata kujiweka kwenye mstari wa kupata dili nyingine

1.Usizulule
Ndugu yangu dunia hii ina mambo mengi sana na ukiaanza kuzulula bila sababu za msingi na hauna  hela ukamwaga nyanya za watu au hata maandazi ya mfanyabaishara wa hapo mataani kwako utalipa na nini na mfukoni una buku tu ya nauli au ya kula jioni utaaibika bure na aibu sio kitu kizuri sana tean ukiwa huna hela ndo mbaya zaidi

2.Usitafute Demu

Kama unaye mmoja tulia naye maana anakupenda na hali yaki hiyo hiyo ila kama unataka kuongeza utajiongezea gharama bure maana atakuomba hela ya kusuka na utakuwa huna tu maan si unajua kabisa huna hela sasa utatoa wapi elfu thelathini ya kumpekea akaweke wivingi mpya aliloliona kwa Diva instagram tena hiyo 30,000 ni makadilio ya chini kuma mitindo ya kusuka hata ya laki mbili na nusu(huu mshahala wa ofsa wa benki unakaa kichwani kwa demu mpya uliyempata Tinder)

3.Usikasirike hovyo

Ndio huna hela alafu unakasirika njaa inaanza kuuma unaanzz kulalamka dunia mbaya wakati hasira zako ndo zimekufanya usikie njaa zisizo na maana vyema kwa muda ambao mfuko wako hauna kitu una njaa kama tumbo lako hakikisha kuwa na furaha muda wote maan furaha ya uso inaweza kumfanya mtu akakupa dili ya hela mchana kweupe (Hasira hasara baba)

4.Usiwe Mchafu

Hata uwe na msoto vipi hakikisha unavaa shati lako safi mambo yaendele hata kama utakuwa umeazima kiatu kwa jilani sawa tu hakikisha unapendeza maana tunaambiwa umalidadi unaficha umaskini kwa hiyo hakikisha ukitoka nje kwenda kutafuta pesa hakikisha umependeza sio unaenda kwenye dili umevaa kama mtu ametoka jalalani bwana utakosa hata hiyo dili na utaendela kuwa na njaa tu mtani kwako.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment