Breaking

Tuesday, April 7, 2020

Mwigizaji Funke wa Nigeria Akamatwa na Polisi Kisa Corona


Mwigizaji Funke Akindele wa Nigeria amekamatwa na Polisi baada ya kufanya house party kusherehekea birthday ya Mume wake ambapo amekamatwa baada ya video kusambaa mtandaoni ikiwaonesha wakila bata ikiwa ni kinyume na agizo la Serikali la kukwepa mikusanyiko kujikinga na corona.

Wawili hawa wamehukumiwa kufanya kazi za kijamii kwa siku 14 na kila mmoja kulipa faini ya Naira ambazo ni sawa na Tsh. 600000, ambapo hata hivyo Funke amerekodi video ya msamaha na kujitetea kwamba Watu wote waliokuwepo kwenye hiyo party wamekua wakiishi kwake kwa siku kadhaa wakirekodi video kwa muda hivyo hakuna alietoka nyumba nyingine kuwafata.

Nigeria imepiga marufuku mikusanyiko ili kujikinga na virusi vya corona ambapo hadi sasa ina Wagonjwa 232, vifo vya Watu watano na waliopona ni 33.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment