Breaking

Wednesday, April 15, 2020

Mwigulu Nchemba "Serikali isitangaze Wagonjwa Wapya wa Covid19"


Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ameishauri Serikali kutangaza idadi ya watu wanaopona au kufariki pekee na kuacha kutangaza idadi ya wagonjwa wapya wa ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19) unaoambukizwa na kirusi cha Corona wanaogundulika kila siku hapa nchini kama ambavyo inafanya sasa

“Mimi naona zibaki taarifa za aina tatu tu, (uwepo wa ugonjwa, waliopona na waliofariki). Hivi tunavyotoa taarifa ni kama nchi zinashindana, sijui kwanini wengine wanatamani takwimu ziwe nyingi na kuwe na wagonjwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa jambo la "kipumbavu" likisemwa kizungu linaonekana la maana, labda kwa sababu Corona ilianzia majuu basi mnaona sifa" Alieleza Nchemba

Tuandikie hapa maoni yako juu ya ushauri huu wa Waziri wa Zamani wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Ndani.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment