Breaking

Thursday, April 23, 2020

‘Ninaamini Kuna Uchawi' Producer wa Msanii Diamond Afunguka

Producer wa msanii wa nyimbo za bongo Diamond Platnumz  Eyo Laizer alisema kuwa anaamini kuna uchawi kwa maana ameuona katika  watu wengi.

Akizungumza na wasafi media alisema kuwa hajawahi kurogwa lakini anaamini kuna uchawi.

“Ninaamini kuna uchawi, nimesikia watu huwa wanatumia uchawi na wengine kurogana, ninaamini hivi vitu viko, sijawahi kurogwa na hata sijawahi  kufikiria kutenda kitendo kama hicho.” Alieleza Lizer.

Lizer alisema kuwa alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu sasa na alitoka kidogo katika kazi ya uzalishaji, mbali na kuugua kwake mashabiki wake walifikiria kuwa alitoka katika lebo ya WCB

Pia alikana madai kuwa alikuwa amesongwa na mawazo.

“Hapana. Sikuwa na mawazo. Nakumbuka vyema nilikuwa mgonjwa na mzalishaji mwingine ndiye alikuwa anafanya kazi yangu

Nilikuwa nyumbani na ndani ya chumba changu kwa muda wa majuma matatu kwa sababu nilikuwa naugua malaria.” Lizer Alisema.

Alisema pia yuko katika lebo ya WCB na ndiye mzalishaji eneo hilo na mkataba wake upo kama kawaida.

Alizidi na kusema kuwa uvumi ambao umekuwa ukiendelea katika mitandao kuwa ametoka katika WCB kwa sababu kwa muda sasa hajakuwa akiposti picha zake na Diamond wakiwa pamoja.

“Mimi si mpiga picha, na sihitaji kuposti picha zangu na Diamond sina hata picha yangu nikiwa na Diamond, ndio mara nyingi huwa nafanya kazi naye, Lakini sikuwangi na wakati wa kupiga picha.” Alizungumza.

Alisema kuwa wimbo ambao ulikuwa mgumu kufanya wakiwa na Diamond ni wa ‘salome’ alioimba Diamond akimshirikisha Rayvanny.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment