Breaking

Monday, April 20, 2020

Pierre Likwidi aeleza alivyopata Corona "Hali Yangu ilikuwa Inatisha Kweli"

Mwanamitandao aliyejipatia umaarufu kwa sababu ya kunywa pombe Pierre Likwidi, amepimwa na amekutwa na maambukizi ya Ugonjwa virusi vya Corona na sasa hivi yupo Karantini katika Hospitali ya Amana iliyopoa Ilala Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Pierre Likwidi amesema anahisi ugonjwa huo aliupata wakati yupo baa.

"Ni kweli nimekutwa na maambukizi ya Corona katika Hospitali ya Temeke, baada ya majibu kutoka tukahamishwa hadi Hospitali ya Amana kwa ajili ya karantini kwa siku 14,  kabla ya kupima hali yangu ilikuwa inatisha kidogo maana nilikuwa na homa kali, kichwa na mwili kuuma sana ila sasa hivi naendelea vizuri" ameeleza Pierre Likwidi.

Pia ameongeza kusema  "Huu ugonjwa nahisi nimepata kwenye baa kwa sababu mimi hakuna sehemu ninayotembelea kama sio baa, huu ugonjwa upo kweli na unaua naomba watu wajikinge sana"

Pierre Likwidi anaungana na msanii wa HipHop Mwana Fa, kuwa watu maarufu ambao wamepatwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment