Breaking

Wednesday, April 22, 2020

Rais Ataka Wananchi Wasimsumbue Mungu “Hawezi Kuwasikiliza Wajinga

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaonya raia wa nchi hiyo kuacha kumsumbua Mungu aliye na mambo mengi kwakua serikali yake imeshatoa muongozo wa namna ya kujikinga na virusi vya Corona

Museveni ametoa kauli hiyo alipokuwa anahutubia taifa siku ya jumapili juu mwenendo wa ugonjwa wa Corona nchini humo

“Tunashukuru Mungu kwa kutulinda maan mpaka leo hakuna kifo hata kimoja kutokana na ugonjwa huu lakini pia tukumbuke Mungu anamambo mengi anayo dunia nzima ya kuiangalia na kuilinda hawezi kuwa hapa Uganda tu akiwaangalia wajinga waliokata kufuata maelekezo ya serikali” amesema Museveni

Mbali na kauli hiyo pia Rais huyo amewataka wananchi wake pia kuacha kusafirisja miili ya watu waliofariki na Corona toka nje kuja kuizika nchini humo kwani kufanya hivyo kuna leta uwezekano wa ugonjwa huo kuendelea kusambaa baina yao.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment