Breaking

Thursday, April 2, 2020

Rihanna Atangaza Kuzaa Watoto Wanne Akitimiza Miaka 42

Kupitia jarida la British Vogue msanii na mfanyabiashara maarufu duniani Rihanna, amefunguka mambo matatu ambayo ni kuhusu muziki wake, kazi na mpango wa kuanzisha familia.

Rihanna ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, ameeleza yupo tayari kuwa mama na kuanzisha familia kwa miaka 10 ijayo, ambapo atakuwa na miaka 42, na anataka kuwa na watoto watatu au wanne.

"Najua nitatakiwa kuishi tofauti kwa wengine na utofauti wenyewe upo kwenye mitazamo ya watoto, ndani ya miaka 10 ijayo nitakuwa na miaka 42 nitakuwa mkongwe kwa mawazo haya nitakuwa na watoto watatu au wanne" ameeleza  Rihanna.

Aidha  ameongeza kusema  "Nahisi kama jamii inataka kuona naishi vile nataka, hakuna mama ambaye atakuwa hana baba wa kuishi na watoto wake, ila kitu ambacho nakitaka ni furaha maana ndiyo utakuwa utajiri pekee kati ya mahusiano ya watoto kwa wazazi, kingine ambacho kitafanya kuwalea watoto ni ukweli na upendo".


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment