Pia ameongeza kuwa utaratibu wa polisi kutumia simu kupiga picha magari yanayokwenda kasi haukubaliki kwa sababu kuna kifaa maalum cha kufanya kazi hiyo.
“Huyu ana Nokia, huyu ana iPhone, huyu ana Samsung, tunaaminianaje, kwamba ni kitendea kazi ambacho tumekipitisha kisheria. Hii haikubali,” amesema.
Simbachawene ameyasema hayo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2020/2021, ambapo amesema vitendo vya polisi kujificha na kuvizia magari, vinaweza kupelekea wao wenyewe kugongwa.
“Kwanini tujifiche? Maana barabarani tupo kila siku, na sisi ndio madereva, sioni sababu ya kujificha. Spidi ziko barabarani mule, tuendelee kuongeza elimu zaidi kwa madereva wetu wapate uelewa na kufuata alama za barabarani,” amesisitiza Simbachawene.
Aidha, amemugiza IGP Simon Sirro kutoa maelekezo maalum juu ya udhibiti wa mwendo wa barabarani kwa sababu kinachofanyika sasa kinaleta fujo.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment