Breaking

Sunday, April 5, 2020

Tanasha Afunguka Uhusiano ‘Mgumu’ na Mama Diamond, Sababu za KuachanaMama mtoto wa Diamond Platinumz, Tanasha Donna amefunguka kuhusu hali ilivyokuwa ndani ya himaya ya msanii huyo, akiwa anaishi kwa ukaribu na mama yake mzazi.

Katika mahojiano aliyofanya na Jarida la ‘True Love’, Tanasha ameeleza jinsi ambavyo hakuwa na uhusiano mzuri na mama mkwe wake, akidai alikuwa anamuonea na kumfanyia ndivyo sivyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya mahojiano hayo iliyoandikwa pia na mtandao wa Ghafla, awali Tanasha alijaribu kuwa mpole akimpa nafasi mama mkwe atawale himaya yote na kwamba hakutaka kufanya lolote litakaloonesha utovu wa nidhamu.

Alidai kuwa ingawa Diamond alikuwa anaangalia kinachoendelea, hakuwahi kumuomba mama yake apunguze kasi dhidi ya Tanasha. Ripoti hiyo inaeleza kuwa Diamond hakuwa anasimama upande wa mpenzi wake huyo hata alipobaini kuwa mama yake hakuwa sahihi wakati mwingine.

Tanasha alithibitisha kuachana na Diamond miezi michache baada ya wawili hao kubarikiwa mtoto.

Taarifa ya kuachana kwao iliwashtua mashabiki wao kwani ilikuwa wakati ambapo wimbo wao mpya ‘Gere’ ulikuwa unafanya vizuri, huku ukiwa kama ishara ya mafanikio zaidi.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment