Breaking

Saturday, April 11, 2020

TBC imepata pigo jingine la kufiwa na wafanyakazi wawili akiwemo mwandishi Haonga
Ikiwa ni takriban siku kumi tangu kumpoteza nguli na mwandishi fundi wa habari Marin Hassan Marin, Shirika la Utangazaji la Tanzania limewapoteza manguli wengine wawili ndani ya Shirika hilo. Marehemu hao ni Joseph Kambanga (Meneja TEHAMA) na mwandishi mwandamizi, Lutengano Haonga.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ameandika “Ni uchungu mkubwa kuwapoteza Joseph Kambanga “Jenerali” (Meneja TEHAMA – TBC) na Lutengano Haonga (Mwandishi wa Habari Mwandamizi – TBC),”.

Aliongezea kuwa “Ni mtihani mzito kwa wana familia wenzangu wa TBC. Laleni salama Kaka zangu, kamwambieni Marin Hassan kuwa ARIDHIO inachanja mbuga.” aliandika Msigwa.

No comments:

Post a Comment