Breaking

Monday, April 27, 2020

UKIYAFANYA Haya Mafanikio Makubwa Yapo Upande Wako

Kwa muda mrefu umekuwa ukijiuliza ni vipi utapata mafanikio unayoyahitaji?  Lakini jibu ni kwamba mafanikio unayo wewe mwenyewe ila tatizo ni kwamba unakuwa ni mtu wa kusuasua kuanza mambo hayo ya kusaka mafanikio. Ngoja nikukumbushe ya kwamba hakuna muda maalumu wa kuyasaka mafanikio. Utawasikia watu wengine wanasema eti nikiwa ukifika miaka 35 au 40 eti ndo utaanza kuyasaka mafanikio kwa kuwa na nyumba, magari na mengineyo. Hii sio kweli  kumbuka ya kwamba muda wa mafanikio ni sasa na wewe ndio mwamuzi wa kuamua  kuanza kuchangamkia fursa zilizopo ili uweze kuwa miongoni  mwa matajiri ambao utakuwa unatajwa midomoni  mwa watu,  naamini  ya kuwa unaweza.

Wapo baadhi ya matajiri wakubwa tunaowajua.  Leo ukijaribu kusoma historia zao wengi wameanza kuwa na mitaji midogo kabisa  lakini leo hii ndio ambao wapo midomoni mwetu. Kwa sisi ambao bado hatujapata mafanikio kwa muda mwingi tunakaa vijiweni tunawajadili , kuwasifia na kuwapa sifa nyingi nzuri bila wao kutusikia hata kutujua majina yetu,  huku wao wakiingiza  fedha na kuzidi kutajirika zaidi. Yapo baadhi ya mambo ambayo leo hii tukiyafanya , sisi  wengine ambao hatuna siri hii ya utajiri  tujijua tutakuwa kama wao.

Yauatayo ndiyo Baadhi ya mambo ambayo leo hii ukiyafanya mafanikio makubwa yatakuwa upande upande wako;

Tenga muda wa kufikiri mambo yako.
Muda ni jambo la msingi sana katika safari ya mafanikio. Kisaikolojia binadamu wote ni sawa ila tunatofautina sana  katika matumizi ya muda. Ngoja nikupe mfano huu ili uweze kunielewa zaidi.  Kwa siku kuna masaa 24. Masaa haya jinsi anavyotumia masikini na tajiri ni tofauti kabisa. Tajiri masaa haya huyaona hayotoshi kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya. Ndo maana hata baadhi ya matajiri ukiwa hufanyi vizuri katika kazi zao utawasikia wanasema usinipotezee muda  maana kwao muda ni mali.

Lakini masaa hayohayo kwa maskini huwa ni masaa mengi sana kwa sababu hana mambo mengi ya kufanya hata kufikiria pia. Maskini huyohuyo akitaka kuamka asubuhi utamsikia anauliza hivi jua limechomoza. Kwa maana ya kwamba yeye huongozwa kwa kulitazama jua. Halikadhalika akiamka asubuhi utamskia usiku wa leo ulikuwa mrefu sana. Ewe  msomaji wa makala haya ukifanya hivo mafanikio utayasikia kwa kina billgate tu.

Jambo la muhimu kumbuka ya kwamba kama kweli umeuchoka na hali ya umaskini hakikisha unatenga muda wa kufikiri mambo ya mafanikio kila siku.  Wakati upo katika muda wa kufikiri mambo yako ya kimafanikio hakikisha ya kwamba unakaa sehemu tulivu ambazo hazina kelele za aina yeyote ile kama vile watoto,  simu, radio, tv na sauti zingine mabazo zitakufanya ufikilie vizuri mambo yako ya muhimu. Pia kumbuka wazo zuri ambalo utalipata lifikirie mwanzo hadi mwisho wa jambo hilo. Pia liwe ni japo moja. Liandike kwenye karatisi au mahali popote ambapo unahisi hatapasau kwa urahisi.

Andika mikakati mizima ya utekezaji wa jambo hilo. Kwa kuangalia zana ambazo zitatumika kuangalia jambo hilo, pia jaribu kutazama changamoto ambazo unahisi zitajitokeza juu ya jambo hilo pamoja na jinsi ya kukabiliana changamoto hizo na jaribu kuona matoteo ya jambo hilo. Kwa ufupi lazima uone maono (VISION) ya wazo lako.

Badili ratiba ya kufanya mambo yako.
Kuna baadhi ya watu tunafanya vitu kimazoe sana hii inapelekea  siku zote tunabaki  vilevile huku tukilalamika ya kuwa maisha ni magumu.

Tukumbuke ya kwamba Kufanya vitu kimazoea kunamfanya mtu asiweze kusongo mbele.
Watu wengi ambao wanalamika juu ya maisha asilimia kubwa utagundua ya kwamba wanafanya vitu kimazoea.  Kama kweli unapenda jambo Fulani la kimafanikio kuwa basi usilifanye  kwa mazoea.
Fanya vitu tofauti na ulivyozoea utaona matokeo makubwa ya kimafanikio yapo upande wako.
Kama umezoe kuamuka saa mbili kamili asubuhi basi amka saa kumi na mbili asubuhi ili uwone mpaka saa mbili utakuwa umefanya nini, kama umezoea kufunga biashara yako saa tatu usiku basi ongeza muda wa kufunga biashara yako hadi saa tano ili uwone kama kuna mabadiliko. Kama wewe ni mvivu basi anza kuwa miongoni mwa watu wanaofanya kazi kwa bidii.

Endapo utafanya hayo yote kwa kuzingatia wewe ni msaka tonge mafanikio makubwa yapo upande wako. Usikate tamaa katika kila jambo unalolifanya. Kuwa shupavu kama simba,  maana simba akikosa nyama hawezi kula nyasi atapambana huku na huko ili apate nyama.

Kama una maswali , ushauri au mapensekezo usisite kuwasiliana na afisa maendeleo na mipango mwandishi wa makala haya  Benson Chonya.  Usisite pia kumshirikisha mwenzako ili aweze kujifunza pia.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment